• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Marekani kuacha kukandamiza kampuni za China bila msingi wowote

    (GMT+08:00) 2019-10-29 19:04:24

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo amesema, China inapinga kithabiti Marekani kukandamiza kampuni za China bila msingi wowote, na kuitaka Marekani kuacha kitendo hicho.

    Bw. Geng Shuang amesema, China imeonyesha msimamo wake mara nyingi kuhusu suala hilo, na inapinga kithabiti Marekani kutumia nguvu za kitaifa kukandamiza kampuni za China bila ushahidi wowote. Kitendo hicho cha umwamba cha Marekani kinaenda kinyume na kanuni yake ya soko huria, pia hakitakubaliwa na jumuiya ya kimataifa.

    Habari zinasema, kamati ya mawasiliano ya simu ya Marekani FCC hivi karibuni imetoa taarifa ikisema itapiga kura dhidi ya miswada miwili kuhusu kampuni za Huawei na ZTE za China, na itaweka vikwazo kwa makampuni ya mawasiliano ya simu ya Marekani kutumia mfuko wa FCC kununua bidhaa za kampuni hizo mbili. Pia inasema vifaa vya kampuni za Huawei na ZTE vinahatarisha usalama wa taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako