• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vietnam yapeleka taarifa Uingereza kuhusu raia wake ambao hawajulikani walipo

    (GMT+08:00) 2019-10-29 19:06:18

    Vietnam imekusanya taarifa zilizotolewa na familia 14 zinazowatafuta ndugu zao walioko Uingereza na kuzituma kwa mamlaka husika nchini Uingereza kwa ajili ya uhakiki.

    Wizara ya Mambo ya Nje ya Vietnam imesema kupitia tovuti yake kuwa, imepokea taarifa kutoka kwa familia hizo ambao wanahitaji msaada baada ya watu 39 kukutwa wamefariki kwenye lori la baridi katika kaunti ya Essex, nchini Uingereza.

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Vietnam Pham Binh Minh amesema, mabadilishano ya taarifa hizo ni kutaka kuhakiki kama taarifa za raia wa Vietnam ambao hawajulikani walipo zinaendana na rekodi za watu waliofariki kwenye lori hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako