Balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Zhang Jun amepinga vikali Marekani na nchi husika kushutumu suala linalohusika na mkoa wa Xinjiang bila msingi wowote kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa.
Bw. Zhang Jun amesisitiza kuwa China inapinga kithabiti kitendo cha Marekani na wenzake kutoa shutuma bila msingi wowote, kuingilia mambo ya ndani ya China, na kuleta uchochezi. Amesema hatua zilizochukuliwa na mkoa wa Xinjiang kujilinda dhidi ya ugaidi na kuondoa itikadi kali zinafuata sheria na maoni ya raia, na si suala la haki ya binadamu, wala hazihusiani na ubaguzi wa kikabila. Amesema China inazitaka Marekani na nchi husika zisiende kinyume na jumuiya ya kimataifa, na wala zisiende mbali zaidi katika njia ya makosa. Pia amesema hakuna nguvu yoyote inayoweza kuzuia maendeleo ya wananchi na taifa la China, na ni hakika kwamba China itakuwa nzuri zaidi katika siku za usoni.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |