• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uhaba mahindi wasukuma juu bei ya unga wa mahindi Dar es Salaam

    (GMT+08:00) 2019-10-30 19:39:10

    Wakazi wa Dar es salaam wamelazimika kuingia zaidi kwa mifuko yao kuweza kununua unga wa mahindi.

    Uchunguzi uliofanywa ulipata maduka mengi katika vitongoji vya Dar, wastani wa bei ya rejareja wa unga wa mahindi kilo moja ni kati ya Tsh1,500 ($ 0.6) na Tsh1,800 ($ 0.7) kutoka Tsh1,000 ($ 0.4) na Tsh1,300 ($ 0.5) katika robo iliyopita ya mwaka huu.

    Takwimu kutoka Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu (NBS) zinaonyesha kuwa katika maeneo ya vijijini bei ya sasa ya rejareja ya unga wa mahindi inayotumiwa na wananchi wengi imeongezeka kidogo kwa kiwango cha wastani cha kati ya Tsh800 ($ 0.3) na Tsh950 ($ 0.4).

    Kushuka kwa bei hiyo kunakuja wakati ambapo Tanzania imepata mavuno mengi kwa mazao ya nafaka katika msimu wa mavuno wa 2017/2018.

    Wasagaji wanakabiliwa na uhaba wa mahindi katika masoko tofauti na imechangiwa na mvua kubwa inayoshuhudiwa hivi sasa katika maeneo mengi nchini, ambayo imeathiri usafirishaji wa mahindi kwenda kwenye vituo kuu vya usagaji .

    Licha ya kuongezeka kidogo kwa bei ya unga wa mahindi, hali ya chakula nchini Tanzania imebakia thabiti kulingana na Waziri wa Kilimo Japhet Hassunga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako