• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda-BRD inalenga kuongeza matumizi ya mfuko wa ukuaji wa mauzo ya nje

  (GMT+08:00) 2019-10-31 19:25:47
  Benki ya Maendeleo ya Rwanda (BRD) inasema kuwa itaongeza uhamasishaji wa mwekezaji kuhusu Mfuko wa Ukuaji wa Mauzo ya Nje huku ikijaribu kuzuia kushuka kwa kasi ya matumizi ya mfuko huo.

  BRD pia inasema itawasaidia wauzaji nje bidhaa kuboresha ustadi wao wa kiufundi ,haswa katika kuunda miradi bora kama sehemu ya juhudi za kuwasaidia kunufaika na mfuko huo na kuongeza mauzo yao.

  Kumekuwa na matumizi madogo ya mfuko huo kutoka kwa makampuni ya usafirishaji nje bidhaa,na BRD imesema hiyo imetokana na ukosefu wa uwezo wa kuunda biashara nzuri ambazo zinaweza kufuzu kwa ufadhili.

  Aidha maafisa wa benki wamesema kuwa kumekuwa na uhamasishaji mdogo na elimu kuhusu bidhaa zinazotolewa chini ya mfuko huo,nah ii ndio sababu ambayo wameanzisha kampeni hiyo ili kushughulikia tatizo hilo.

  Chini ya kampeni hiyo,benki ya BRD itaongeza juhudi zinazolenga kuwafikia wasafirishaji wa bidhaa na kuwaonyesha fursa za ufadhili wa kifedha ambazo mfuko huo zinatoa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako