• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kampuni ya Umeme ya Kenya Power yarudia matumizi ya magogo ya miti

  (GMT+08:00) 2019-10-31 19:26:08
  Kampuni ya umeme nchini Kenya (Kenya Power) imeonyesha nia ya kununua miti ya Eucalyptus kwa ajili ya miradi yake ya usambazaji umeme.

  Katika notisi ya umma iliyochapishwa kwenye magazeti nchini Kenya,kampuni hiyo imewaalika wakuzaji miti kwa ajili ya biashara kutuma maombi ya zabuni ya miti iliyokomaa ambayo itatumiwa kama nguzo za umeme.

  Notisi hiyo ilisema kuwa kampuni ya Kenya Power inafanya utafiti wa upatikanaji wa miti iliyokomaa aina ya Eucalyptus kwa ajili ya matumizi ya miradi ya usambazaji umeme.

  Habari hiyo imekuwa neema kwa wakulima wa miti ya eucalyptus ambao walipata hasara ya mamilioni ya pesa kwa miaka kadhaa baada ya kampuni ya Kenya Power na Mamlaka ya Usambazaji Umeme Vijijini kupunguza matumizi ya magogo ya miti ili kugeuza mienendo ya ukataji miti.

  Wakulima walio na mashamba ya miti yenye umri wa miaka 10 na kuendelea wanaweza kutuma maombi yao kufikia Oktoba 31.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako