• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga Uingereza kuingilia mara kwa mara mambo ya Hong Kong

    (GMT+08:00) 2019-11-01 08:40:59

    Ofisi ya kamishna wa wizara ya mambo ya nje ya China kwenye mkoa wa utawala maalum wa Hong Kong, imeeleza kupinga vikali kitendo cha Uingereza kuingilia mara kwa mara mambo ya Hong Kong.

    Kwenye taarifa iliyotolewa baada ya Uingereza kutoa ripoti nyingine ya "miezi sita kuhusu hali ya Hong Kong", msemaji wa ofisi hiyo amesema mambo ya Hong Kong ni mambo ya ndani ya China na inapinga kitendo cha Uingereza kuingilia mambo ya Hong Kong kwa kutoa ripoti kama hiyo.

    Amesema sera za "nchi moja, mifumo miwili" na "wahong kong waitawala Hong Kong" zimetekelezwa kwa miaka 22 iliyopita tangu Hong Kong irudi China, na mtu yeyote asiye na upendeleo wa kisiasa atatambua hilo.

    Amesema ripoti hiyo inaenda kinyume na maoni ya umma yanayotaka kukomesha kwa vurugu, kurudisha utawala wa sheria na utaratibu, na Uingereza kuheshimu mamlaka ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako