• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IGAD yaihimiza Sudan Kusini ielekeze mapato ya mafuta kwenye mchakato wa amani

    (GMT+08:00) 2019-11-01 09:23:22

    Jumuiya ya maendeleo ya kiserikali ya nchi za Afrika Mashariki (IGAD) jana imeihimiza Sudan Kusini ielekeze mapato ya mafuta kwenye utekelezaji wa makubaliano ya amani, yaliyosainiwa mwezi Septemba mwaka jana na pande zinazovutana.

    Mkurugenzi wa Ofisi ya Juba ya jumuiya ya IGAD Bw. Esfaye Negassa amesema, mapato yanayotokana na uuzaji wa mafuta nje yanaweza kusaidia ukarabati wa nchi hiyo.

    Mwakilishi maalumu wa Kenya anayeshughulikia suala la Sudan Kusini Bw. Kalonzo Musyoka, amesema Sudan Kusini haipaswi kutumia vibaya fursa ya kutimiza amani na utulivu wa muda mrefu, na inapaswa kutumia maliasili mbalimbali kama mafuta na gesi katika kuhimiza ujenzi wa amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako