• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RAGA: Kikosi cha Shujaa kuanza kampeni za kufuzu Olimpiki Tokyo

    (GMT+08:00) 2019-11-01 09:55:07

    Kikosi cha Kenya cha wachezaji saba kila upande, Shujaa, kitafungua kampeni za kufuzu kwa Olimpiki za Tokyo 2020 dhidi ya Ivory Coast mnamo Novemba 2019 jijini Johannesburg, Afrika Kusini. Zimbabwe ambao ni mabingwa wa Africa Sevens, watapimana nguvu na Nigeria huku Uganda wakipangwa kuvaana na Mauritius. Katika mechi nyinginezo za raundi ya kwanza, Madagascar watamenyana na Botswana, Zambia wachuane na Ghana, Tunisia wakwaruzane na Namibia huku Senegal wakionana na Morocco. Kwa mujibu wa Shirikisho la Raga la Afrika, mfumo tofauti utatumika katika mashindano ya mwaka huu ambayo yataleta mataifa 14 tofauti ambayo yameorodheshwa kulingana na matokeo yao ya mwaka uliopita. Ili kujifua vilivyo kwa kampeni hizo, wanaraga wa Kenya tayari wameingia kambini mwa mazoezi ya siku nne. Wengi wao ni wale waliounga kikosi cha Kenya Morans kilichowazamisha Afrika Kusini 19-14 majuma mawili yaliyopita na kunyakua taji la Safari Sevens.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako