• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Jurgen Klopp atishia kutoipeleka timu yake kucheza dhidi ya Aston Villa hatua ya robo fainali Kombe la Carabao

    (GMT+08:00) 2019-11-01 09:55:32

    Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ametishia kuwa hatoipeleka timu yake kucheza mchezo wa hatua ya robo fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Aston Villa. Klopp amesema kuwa endapo tarehe ya ratiba ya michuano hiyo haitabadilika, hawatacheza mechi yao na kwa maana hiyo ushindi utakwenda kwa wapinzani wao. Amesisitiza kuwa vitu kama hivi vinatakiwa kuangaliwa kwa umakini, kwani timu moja haiwezi kuwa sehemu ya michezo yote kwa wakati mmoja. Liverpool inakabiliwa na ratiba ya michezo 10 katika kipindi cha mwezi Disemba, ambapo Disemba 4 itavaana na Everton katika ligi kabla ya kucheza na Bournemouth Disemba 7. Itasafiri hadi nchini Austria kucheza na RB Salzburg, Disemba 10 katika mchezo wa Klabu Bingwa Ulaya kabla ya kurejea nyumbani kucheza na Watford, Disemba 14 katika ligi. Disemba 16 itacheza na Aston Villa katika ligi kabla ya kusafiri hadi nchini Qatar kucheza michezo miwili ya Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia hadi Disemba 21 kisha kurejea nyumbani kucheza na Leicester City, Wolves na Sheffield United.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako