• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Yanga yaifuata Pyramids ikiwa na kibarua kikubwa mbele yake

    (GMT+08:00) 2019-11-01 09:55:59

    Kikosi cha Yanga SC kimeondoka jana jioni mjini Dar es Salaam kwenda Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano, mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Pyramids FC utakaochezwa Jumapili wiki hii Uwanja wa Jeshi la Anga wa Juni 30 mjini Cairo.

    Yanga inatakiwa kushinda 2-0 ugenini au kushinda kwa tofauti ya bao moja kuanzia 3-2 kwenye mchezo huo utakaoanza Saa 4:00 usiku, kufuatia kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Jumapili iliyopita Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza. Huo ulikuwa mwendelezo wa rekodi ya Yanga kutoshinda nyumbani mechi za michuano ya Afrika kuanzia Ligi ya Mabingwa ambako ushindi wa ugenini wa 1-0 uliwavusha Raundi ya pili baadaye sare ya 1-1 nyumbani na Township Rollers kabla ya kwenda kutolewa na Zesco United kufuatia kufungwa 2-1 Ndola ikitoka sare ya 1-1 Dar es Salaam.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako