• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KIKAPU: Rwanda kuwa mwenyeji wa michuano ya raundi ya pili ya BAL Qualifiers

    (GMT+08:00) 2019-11-01 09:57:18

    Rwanda imethibitisha kuwa moja kati ya nchi mbili zinazoandaa michuano ya raundi ya pili ya kufuzu Ligi ya Basketball Africa (BAL). Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Rwanda (Ferwaba) Désiré Mugwiza amethibitisha hayo jana wakati anaongea na wanahabari. Michuano ya raundi ya pili na ya mwisho itafanyika kuanzia Novemba 26 na kumalizika Disemba 1. Timu 16 zitagawanywa kwenye makundi mawili ambayo yatakuwa na timu nane. Timu sita bora zitajiunga moja kwa moja na klabu bingwa kutoka Angola, Misri, Morocco, Nigeria, Senegal, na Tunisia kushindana kwenye michuano ya Ligi ya Afrika 2020 ambayo kawaida inakuwa na jumla ya timu 12. Wakati michezo ya raundi ya pili ikiwa bado haijafanyika, Rwanda itakuwa mwenyeji wa kundi moja huku kundi jingine likifanya mechi zake nchini Cameroon. Fewaba iliomba kuandaa michuano ya raundi ya pili siku kadhaa zilizopita baada ya mabingwa wa nchi hiyo Patriots kumaliza kileleni kwenye kundi D katika mechi za raundi ya kwanza zilizochezwa Dar es Salaam, Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako