• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Ndayiragije ajifungia kuwasoma Guinea Ikweta

    (GMT+08:00) 2019-11-01 17:51:59
    Wakati Taifa Stars ikijipanga kucheza na Guinea ya Ikweta katika mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2021), kocha wa timu hiyo, Etienne Ndayiragije, amesema anaendelea kuwasoma wapinzani wao kupitia mikanda ya video kutokana na michezo waliyocheza hivi karibuni. Taifa Stars inatarajia kucheza na Guinea ya Ikweta, Novemba 15, mwaka huu, jijini Dar es Salaam. Ndayiragije aliyekuwa kaimu kocha mkuu wa Stars, baada ya Emmanuel Amunike kutimuliwa Julai mwaka huu, tayari ameiwezesha timu hiyo kutinga makundi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar. Kocha huyo, pia ameiwezesha Stars kufuzu kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi ya Ndani (CHAN) zitakazofanyika.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako