• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwenendo wa Stamico wasifiwa

    (GMT+08:00) 2019-11-01 18:12:24

    Waziri wa Madini wa Tanzania, Doto Biteko amesema mwenendo wa Shirika la Madini la Taifa nchini humo (Stamico) ni mzuri kwa sasa ikilinganishwa na kipindi cha nyuma.

    Akizungumza mbele ya kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Bw Biteko amesema shirika la Stamico lina uwezo wa kutoa gawio kwa Serikali la Sh1 bilioni, hivyo ameiomba kamati hiyo kuendelea kuiunga mkono wizara yake katika mipango ya kulisimamia na kulifanya kuwa na tija kama inavyotarajiwa.

    Amesema matatizo makubwa yanayoifanya Stamico kushindwa kwenda kwa kasi kama inavyo tarajiwa, yamewasilishwa kwenye kamati hiyo na mamlaka nyingine ili kupatiwa ufumbuzi.

    Waziri Biteko amesema kwa sasa usimamizi wa miradi ya shirika hilo inaonyesha kuwa na tija huku akitolea mfano mgodi wa TAMIGOLD unaomilikiwa na Stamico kwa niaba ya Serikali, ambao unatengeneza faida tofauti na zamani.

    Amesema pia gharama za uendeshaji wa mgodi huo zimepungua kutoka Dola 1,800 kwa wakia moja hadi Dola 940 kwa wakia moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako