• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfumuko wa bei waongezeka Kenya

    (GMT+08:00) 2019-11-01 18:24:39

    Mfumuko wa bei nchini Kenya umeongezeka kwa asilimia 4.95 kwa bidhaa za chakula jambo ambalo limesababisha kupanda kwa gharama ya maisha. Idara ya takwimu nchini Kenya imesema ongezeko hilo ambalo kwa miezi 18 iliyopita ilikuwa ni asilimia 3.83 imechangiwa na kupanda kwa bei ya bidhaa kama vile sigara kutokana na kupanda kwa kodi. Bei ya bidhaa nyingi za chakula ziliongezeka katika mwezi wa Septemba ikilinganishwa na mwezi wa Agosti. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu mkuu mtendaji wa Idara ya Takwimu Zachary Mwangi, bei ya unga wa mahindi na tomato iliongezeka kwa asilimia 5.42 na 4.58 mtawalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako