• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Kusini yatarajia kupanua soko la China kwa kupitia CIIE

    (GMT+08:00) 2019-11-03 18:16:56

    Maonyesho ya pili ya kimataifa ya uagizaji wa bidhaa yatafunguliwa Jumanne ijayo mjini Shanghai.

    Kwenye maonyesho hayo, maeneo ya kuonyesha chakula na bidhaa za kilimo yatakuwa maeneo makubwa kabisa ya kampuni zitakazoshiriki kwenye maonyesho hayo, ambapo chakula kutoka sehemu mbalimbali duniani kinatarajiwa kuwekwa mezani, ikiwemo nyama ya ng'ombe ya Afrika Kusini.

    Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Beefmaster ya Afrika Kusini Bw. Gert Blignaut amesema kuwa kampuni yake inatilia maanani soko la China, ambapo itashiriki kikamilifu maonyesho hayo na kutarajia kutangaza nyama ya ng'ombe kupitia jukwaa la maonyesho hayo.

    Bw. Gert ameongeza kuwa maonyesho hayo ni ya kipekee na ni jukwaa la biashara, ambayo yanasaidia kuwasiliana na wateja, kupata fursa ya biashara, na kupata wateja wengi zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako