• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Eliud Kipchoge na Brigid Kosgei wanyakua mataji New York

    (GMT+08:00) 2019-11-04 08:44:42

    Wanariadha bingwa wa Kenya Eliud Kipchoge na Brigid Kosgei wamekabidhiwa tuzo ya Abbott World Marathon Majors Series XII. Kipchoge aliwapiku washindani wenzake kutoka Ethiopia Lelisa Desisa na Birhanu Legese kutia kikapuni tuzo hiyo maridadi baada ya kujizolea alama 50. Desisa na Legese walipata alama 41 kila mmoja, lakini walichukuwa nafasi za pili kufuatia kura kutoka kwa wakurugenzi wa hafla hiyo. Katika kitengo cha akina dada, Kosgei, ambaye pia alijizolea alama 50, aliwabwaga wanariadha matata wa Ethiopia Ruti Aga na mwenzake Vivian Cheruiyot na kujipatia taji hilo. Aga na Cheruiyot walimaliza katika nafasi ya pili na tatu mtawalia. Ushindi wa tuzo hizo utawashuhudia Kipchoge na Kosgei wakitia kibindoni kima cha KSh 25 milioni kila mmoja kama zawadi ya ushindi wao. Wawili hao walikumbana na kampeni kali huku wote wakishinda mbio za Virgin Money London Marathon mnamo mwezi Aprili mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako