• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya voliboli ya kuketi ya Rwanda kwa wanawake yaelekea Japan kwenye michuano ya Mabingwa ya World Super 6

    (GMT+08:00) 2019-11-04 08:45:07

    Timu ya taifa ya mpira wa wavu wa kuketi ya wanawake ya Rwanda imeondoka kuelekea Japan, kushiriki michuano ya Mabingwa ya World Super 6 2019. Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza November 12 na kumalizika 17. Kwa mujibu wa Kamati ya Taifa ya wachezaji walemavu, kabla ya michuano timu itakuwa na mazoezi makali ya wiki nzima huko Okinawa. Naye kocha msaidizi Jean-Marie Nsengiyumva amesema kambi ya mzoezi itawasaidia wachezaji kuwa na hamu ya mashindano na kujiongeza zaidi. Mashindano ya World Super 6 yanazileta pamoja timu sita bora duniani za wanawake wanaocheza mpira wa wavu wa kuketi. Rwanda itakuwa inawalikilisha bara la Afrika baada ya kushinda ubingwa wa dunia mwezi Septemba na kujikatia tiketi kwenye mashindano hayo baada ya kuishinda Misri kwenye uwanja Amahoro Stadium.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako