• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri mkuu wa China akutana na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa

  (GMT+08:00) 2019-11-04 09:06:38

  Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana huko Bangkok alikutana na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres.

  Bw. Li Keqiang amesema, kwa sasa hali ya kimataifa imebadilika sana, China ikiwa ni nchi mjumbe wa kudumu wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, itaendelea kushikilia kulinda utaratibu wa pande nyingi, kulinda mfumo wa kimataifa ambao kiini chake ni Umoja wa Mataifa, kulinda utaratibu wa kimataifa wenye msingi wa sheria ya kimataifa. Amesema China pia inapenda kuzidisha ushirikiano na Umoja wa Mataifa, kuunga mkono kazi ya katibu mkuu, kushirikiana na pande mbalimbali kutekeleza ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030.

  Bw. Guterres amesema, maendeleo ya China yanasaidia mchakato wa dunia yenye ncha nyingi na hali yenye pande nyingi, pia yanasaidia amani ya dunia. Umoja wa Mataifa inapongeza mchango uliotolewa na China katika kuunga mkono utaratibu wa pande nyingi na utaratibu wa kimataifa kwenye msingi wa sheria ya kimataifa, kutekeleza ajenda ya mwaka 2030 na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Pia amesema, sekretarieti ya Umoja wa Mataifa inaunga mkono pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako