• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makampuni yanayotoa utoaji wa huduma za biashara yafanya maandalizi kushiriki kwenye Maonesho ya pili ya CIIE

    (GMT+08:00) 2019-11-04 17:45:08

    Maonesho ya pili ya uagizaji bidhaa ya kimataifa ya China CIIE yataanza kesho huko Shanghai. Kutokana na kwamba maonesho ya kwanza yalipata mafanikio mazuri, maonesho ya pili yanafuatiliwa sana na watu duniani, na yatashirikisha makampuni zaidi ya elfu tatu kutoka nchi na sehemu 150 kote duniani. Je, makampuni hayo yatatoa bidhaa na mipango gani kwenye maonesho hayo?

    Mkuu wa Kampuni ya uhasibu ya Deloitte, ambayo ni moja kati ya makampuni maarufu manne ya mambo ya uhasibu duniani, bibi Liu Minghua anasema:

    "Hivi sasa ni vigumu sana kwa kupata nafasi ya kushiriki kwenye Maonesho haya. Kampuni yetu ilipata mafanikio mazuri kwenye maonesho hayo ya kwanza, ushawishi wa chapa yetu uliongezeka na matangazo yalizidi kuimarishwa, ndiyo maana katika maonesho haya ya pili tumeongeza mara mbili eneo la kampuni yetu."

    Naibu meneja mkuu wa idara ya soko la China, maendeleo na mikakati iliyo chini ya Kampuni ya TUV ya Ujerumani, ambayo ni kampuni inayoongoza duniani kwa utoaji wa upimaji na ushirikisho, Bw. Li Tao anasema:

    "Bidhaa zetu zote zinatimizwa kwa utoaji wa teknolojia. Mwaka huu tunaleta utoaji wa huduma zenye umaalumu, kama vile tutazingatia sekta ya uhifadhi wa mazingira ya kushughulikia taka. Tutatoa huduma za upimaji na uthibitisho wa kupunguza madhara ya vitu vinavyotumiwa kutengenezea mifuko ya plastiki, ili kueneza matumizi ya mifuko hiyo."

    Pia anaona kuwa maonesho hayo ni jukwaa la kushirikisha bidhaa zote bora duniani katika mchakato wa utengenezaji wa China, na yana umuhimu mkubwa.

    Wakati wa maonesho hayo, makampuni mengi yanayotoa huduma mbalimbali za biashara, yataonesha mipango mipya na ya kisasa, na pia kuonesha matumaini makubwa juu ya matokeo yatakayopatikana kwenye maonesho hayo. Bi. Liu Minghua anasema:

    "Huu ni mwaka wa 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China. Mvuto wa China kwa uwekezaji wa wafanyabiashara wa ng'ambo umekuwa ukiongezeka siku hadi siku. Maonesho hayo yatakuwa daraja la kuoanisha mambo ya kidiplomasia, mawazo ya jopo la washauri bingwa na shughuli kati ya makampuni kati ya nchi mbalimbali duniani. Nayatakia maonesho hayo ya pili yatapata mafanikio mazuri, na tutanufaika kwa pamoja katika zama mpya."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako