• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vietnam yasema ujumbe wake unashirikiana na mamlaka za Uingereza kuitambua haraka miili ya watu iliyokutwa kwenye lori

    (GMT+08:00) 2019-11-04 18:38:59

    Ujumbe wa Wizara ya Usalama wa Umma kutoka Vietnam unashirikiana na mamlaka za nchini Uingereza kuitambua kwa haraka miili ya watu iliyokutwa ndani ya lori moja la baridi huko Essex, ambako inaaminika wahanga wengi ni raia wa Vietnam.

    Waziri wa wizara hiyo To Lam amesema, ujumbe huo uliwasili nchini Uingereza jana na ulitarajiwa kutuma ripoti ya kwanza leo mchana. Amesema ujumbe huo umechukua taarifa nyingi za uhakika zinazohusiana na familia zilizotoa taarifa za kupotea kwa ndugu zao ili kuhakiki na upande wa Uingereza. Amesema mara maiti za Wavietnam zitakapotambuliwa, wizara yake itachukua hatua za ulinzi kwa raia na kushirikiana na taasisi nyingine za serikali kusafirisha miili hiyo nyumbani. Pia itaendelea na uchunguzi ili kuwafikisha waliohusika na tukio hilo mbele ya sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako