• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa 35 wa kilele wa ASEAN wafanyika Thailand

    (GMT+08:00) 2019-11-04 19:06:12

    Mkutano wa 35 wa kilele wa Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini na Mashariki (ASEAN) na mikutano ya viongozi kuhusu ushirikiano wa nchi za Asia Mashariki imefunguliwa jana nchini Thailand.

    Viongozi kutoka nchi 10 za ASEAN na nchi 8 washirika wa mazungumzo ya Jumuiya hiyo wameshiriki kwenye mikutano hiyo, na kujadiliana masuala juu ya ujenzi wa ASEAN, maendeleo endelevu, na kuimarisha mazungumzo na nchi washirika.

    Akihutubia ufunguzi wa mkutano huo, waziri mkuu wa Thailand Bw. Prayuth Chan-ocha amesema nchi za ASEAN zitachukua hatua za pamoja katika kudumisha amani na utulivu na kuhimiza maendeleo endelevu ya uchumi wa kanda hiyo. Ametoa wito kwa pande zote husika kukamilisha mazungumzo juu ya makubaliano ya uhusiano wa wenzi wa kiuchumi wa pande zote wa kikanda ndani ya mwaka huu, na kuhimiza maendeleo ya uchumi wa kikanda na biashara ya pande nyingi chini ya mfumo wa WTO.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako