Ofisa wa mambo ya huduma za biashara kutoka Kituo cha biashara ya dunia cha Umoja wa Mataifa Bw. Zhao Quan amesema, kituo hicho kitaongoza makampuni 100 ya nchi zinazoendelea kushiriki kwenye maonyesho ya pili ya kimataifa ya uingizaji bidhaa kutoka nje ya China (CIIE) yatakaofunguliwa kesho mjini Shanghai, ili kuyapatia fursa zaidi ya kuuza nje bidhaa zao.
Bw. Zhao amesema maonyesho hayo ni moja ya hatua muhimu za kufungua mlango, na yataziletea nchi nyingi fursa za kuuza bidhaa kwa China, na kuwapatia watu fursa nyingi za ajira. Ameongeza kuwa mafanikio mengi yamepatikana nchini China kwenye sekta ya uagizaji na kuuza bidhaa nje.
Amesema China inashikilia kufungua mlango na kuweka sera nyingi kwenye sekta za huduma na biashara ikiwa ni pamoja na fedha na mawasiliano ya simu, hatua itakayoiongoza China kuingia kwenye kipindi kipya cha maendeleo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |