• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China akutana na mwenzake wa Japan

    (GMT+08:00) 2019-11-04 19:07:37

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang leo amekutana na mwenzake wa Japan Bw. Shinzo Abe kando ya mkutano wa 22 wa viongozi kati ya China, Korea Kusini, Japan na jumuiya ya ASEAN uliofanyika leo mjini Bangkok, Thailand.

    Bw. Li amesema, China na Japan zikiwa ni nchi kuu za kundi la uchumi duniani, zina matumaini ya pamoja katika kulinda utaratibu wa dunia yenye ncha nyingi na biashara huria. Amesema nchi hizo zinapaswa kutekeleza nyaraka nne za kisiasa kati yao, kuheshimu maslahi makuu na ufuatiliaji mkuu wa upande mwingine, kutatua masuala nyeti kwa njia mwafaka, kuongeza kiwango cha uaminifu, na kuweka uhusiano mzuri zaidi wa kudumu wenye utulivu. Ameongeza kuwa mwaka huu inatimia miaka 20 tangu kuanzishwa kwa ushirikiano kati ya China, Japan na Korea Kusini, na China itaitisha mkutano wa nane wa viongozi wa nchi hizo tatu, ikitarajia mkutano huo utahimiza ushirikiano wa pande zote, na kulinda utulivu na ustawi wa kanda hiyo kwa pamoja.

    Naye Shinzo Abe amesema Japan inapenda kuimiarisha mawasiliano na China, kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji, na kudumisha uratibu juu ya mambo ya kimataifa na ya kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako