• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mfumuko wa bei wa chakula uko chini nchini Uganda licha ya mavuno duni

  (GMT+08:00) 2019-11-04 19:47:48

  Licha ya mavuno duni kutoka msimu wa kwanza wa mazao wa 2019 Uganda imedumisha kiwango cha chini cha mfumko wa bei ya chakula kwa asilimia 1.9 kutoka mavuno makubwa ya mwaka wa 2018.

  Nchi ilipata mavuno makubwa ya mahindi, maharagwe, mchele wa mtama; mihogo, viazi vitamu, na viazi vya Ireland ambayo imeshikilia bei ya vyakula vyote vikuu kutoka Juni 2018.

  Ujumbe wa hivi karibuni wa Shirika la Chakula na Kilimo nchini Uganda unasema, Jumla ya uzalishaji wa nafaka kwa mwaka wa 2019 umewekwa kwa kiwango cha tani milioni 3.4, karibu asilimia 10 kutoka 2018 na asilimia 5 chini ya wastani wa miaka mitano iliyopita, hata hivyo mfumko wa chakula inatarajiwa kupungua mnamo Desemba wakati mavuno mapya yatakuwa yakifikia masoko.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako