Kamati ya taifa ya kupambana na majanga ya Ethiopia na Shirika la mpango wa Chakula la Umoja wa mataifa WFP, wamezindua mkutano wa dunia wenye lengo la kutokomeza njaa duniani.
Mkutano huo unaofanyika mjini Addis Ababa unatokana na mahitaji ya njia ya kushughulikia matatizo kwenye mfumo wa chakula duniani, yanayotatiza juhudi za kutokomeza njaa kabla ya mwaka 2030.
Mkutano huo unaofanyika wakati watu milioni 820 duniani wanasumbuliwa na njaa, na milioni 125 kati yao wanasumbuliwa na njaa kali.
Mkutano huo umewaleta pamoja watunga sera wanaowajibika na maswala ya chakula na lishe, watoa misaada ya chakula, wafadhili, wahisani na wanataaluma wa usalama wa chakula.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |