• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kikosi cha Afrika Mashariki chaanza luteka ya pamoja nchini Uganda

  (GMT+08:00) 2019-11-05 09:11:56

  Askari zaidi 360 kutoka nchi 6 wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC wameanza luteka ya pamoja ya wiki mbili katika eneo la Jinja mashariki mwa Uganda.

  Naibu msemaji wa jeshi la Uganda Deo Akiiki amesema luteka hiyo ya CPX inalenga kuhimiza ajenda ya mafungamano ya kikanda na ushirikiano wa majeshi ya kanda hiyo, pia kuimarisha uwezo wao wa kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiusalama katika kanda hiyo.

  Luteka hii ya 12 yenye jina la "Ushirikiano Imara 2019" inashirikisha watu kutoka jeshi, polisi, magereza, idara za uhamiaji na wadau wa kiraia wa Uganda, Rwanda, Tanzania, Burundi, Kenya na Sudan Kusini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako