• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China ashiriki kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za Asia Mashariki

    (GMT+08:00) 2019-11-05 17:41:12

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana ameshiriki kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za Asia Mashariki uliofanyika mjini Bangkok, Thailand.

    Li amesema, hali ya sasa ya kimataifa inabadilika mara kwa mara, huku msukumo wa kuhimiza ukuaji wa uchumi wa dunia ukipungua, jambo linaloziletea nchi za Asia Mashariki athari mbaya. Mkutano huo wa wakuu wa nchi za Asia Mashariki unashikilia kuhimiza ushirikiano wa usalama na wa siasa, maendeleo ya uchumi na jamii, mawasiliano ya kimkakati, na ushirikiano wa kiutendaji.

    Amependekeza kuwa nchi husika zinapaswa kushikilia ushirikiano wa kunufaishana, kujenga uchumi wa dunia ya ufunguaji mlango kwa pamoja, kuhimiza maendeleo na kutimiza ustawi wa pamoja, pia kushikilia ushirikiano wa aina mpya wa kiusalama na kulinda usalama kwa pamoja.

    Bw. Li Keqiang pia amehudhuria mkutano wa tatu wa viongozi juu ya makubaliano ya ushirikiano wa wenzi wa kiuchumi wa pande zote wa kikanda RCEP mjini Bangkok.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako