• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi mbalimbali zashiriki kwenye maonyesho ya pili ya CIIE

    (GMT+08:00) 2019-11-05 19:13:29

    Maonyesho ya Pili ya Kimataifa ya Uingizaji Bidhaa kutoka nje ya China (CIIE) yamefunguliwa leo mjini Shanghai, na yanashirikisha makampuni zaidi ya elfu tatu kutoka nchi na sehemu 150 kote duniani.

    Kenya ni nchi ya pili ya uzalishaji wa parichichi barani Afrika, pia ni nchi ya tano duniani na nchi ya kwanza barani Afrika kuruhusiwa kuuza parachichi nchini China. Kampuni ya kilimo ya Vertical ya Kenya ni kampuni kubwa zaidi nchini Kenya inayouza parachichi zinazogandishwa kwa nchi za nje, na tayari kilo 200 za parachichi zimepelekwa mjini Shanghai, China mwezi Septemba mwaka huu. Ofisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Bw. Hasit Shah amesema China ina soko na uwezo mkubwa. Amesema,

    "Siku zote nchi za Afrika zina wazo baya kuwa biashara ya China ni kwa upande mmoja. Lakini, hivi sasa tunaona kwamba China inafungua mlango kwa dunia nzima. China ni soko kubwa zaidi duniani, ina kundi kubwa la watu wa tabaka la kati. Hivyo tuna matumaini makubwa sana, lazima tutoe bidhaa zenye ubora na bei nafuu."

    Vyakula ni bidhaa kuu za Uturuki zitakazoonyesha kwenye maonyesho hayo. Naibu mwenyekiti wa Shirikisho la makampuni ya uuzaji wa bidhaa nje la Aegean la Uturuki Bw. Birol Celep amesema, China ina soko kubwa lenye watu bilioni 1.4, ambao wanafuatilia zaidi ubora wa maisha. Kampuni yake imefuatilia soko la China kwa siku nyingi na kufanya maandalizi mengi ya kuingia kwenye soko hilo. Mkurugenzi wa kampuni hiyo tawi la China Bw. Neset Kececiogullari amesema, kampuni yao imekusanya maoni ya watu wa China kwa miaka kadhaa, ili kuboresha bidhaa zao zitakazouzwa nchini China. Amesema,

    "Mwaka jana, tulileta matunda yaliyokaushwa nchini China, na kupata maoni kutoka wateja wa China. Tutatumia mfuko mdogo zaidi wa chakula mwaka huu, kulingana na uzoefu wa wateja wa China. Tunatumai tutapewa majibu mengi zaidi kutoka kwao."

    Makampuni 15 ya Iran yatashiriki kwenye maonyesho hayo na kuweka vibanda 20 vya bidhaa, ikiwa ni pamoja na sekta za biashara ya kidigitali, kilimo, sanaa na nyinginezo. Ofisa mkuu mtendaji wa kampuni ya kidigitali ya Sedna ya Iran Bw. Hadi Ghazzaghi amesema, kampuni yake inatilia maanani sana fursa hiyo, na wamefanya maandalizi mapema sana. Amesema,

    "Kwa nchi nyingi duniani, maonyesho haya ni makubwa zaidi ya kuuza bidhaa zao kwa China, na yanayavutia makampuni mengi ya dunia na kusifiwa nayo mara kwa mara. Makampuni mengi ya Iran yanataka kushiriki kwenye maonyesho hayo, na kuwavutia wateja wengi zaidi na kutafuta wenzi wa ushirikiano. Tunaona kuwa maonyesho haya yana ushawishi mkubwa, ni muhimu kwenye sekta ya maonyesho ya aina hiyo."

    Takwimu kutoka shirikisho la wafanyabiashara na viwanda la Ujerumani zimeonyesha kuwa, makampuni 205 ya Ujerumani yanashiriki kwenye maonyesho hayo. Mkuu wa shirikisho hilo anayeshughulikia mambo ya Asia Mashariki Bibi Vera Philipps amesema, shirikisho hilo litahimiza makampuni ya Ujerumani yatumie vizuri fursa hiyo ya kuonyesha huduma na bidhaa zao. Amesema,

    "Maonesho hayo ni maonesho ya kwanza duniani yenye madhumuni ya uingizaji bidhaa kutoka nje, na yanatoa fursa nzuri kwa makampuni ya nchi mbalimbali katika kuingia au kuimarisha masoko yao nchini China. Ujerumani ni mwenzi muhimu zaidi wa biashara wa China barani Ulaya, aidha, China ni nchi mshirika wa kwanza wa uchumi kwa Ujerumani barani Asia. Hivi sasa China imekuwa mwenzi mkubwa zaidi wa bishara wa Ujerumani katika miaka mitatu mfululizo. Hivyo, tunaamini kuwa maonesho hayo yatahimiza zaidi maendeleo ya uhusiano wa uchumi na biashara kati ya China na Ujerumani."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako