• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mabingwa wa kombe la dunia la Raga wapata mapokezi makubwa walipowasili Johannesburg

  (GMT+08:00) 2019-11-06 09:05:18

  Nahodha wa Springboks Siya Kolisi amesema ushindi wao wa Kombe la Dunia la Raga ni kwa ajili ya Waafrika Kusini wote wanaoifanya nchi hiyo iwe mahali pazuri. Kolisi amekuwa nahodha wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini kubeba Kombe la William Webb Ellis wakati Springboks ilipoishinda England 32-12 Jumamosi. Kiliporejea nyumbani kikosi cha Springboks kilipata mapokezi makubwa ambapo maelfu ya mashabiki walifika kukilaki kilipowasili Johannesburg jana. Wachezaji waliwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa OR Tambo kwa ndege tatu tofauti, ambapo wengine wanatarajiwa kuwasili leo. Kikosi hicho kinatarajiwa kufanya ziara ya mabingwa 'Champions Tour' ambapo watatembelea Durban, East London, Port Elizabeth and Cape Town, baada ya maandamano katika miji ya Pretoria, Johannesburg na Soweto kesho Alhamisi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako