• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maofisa wa riadha wa Japan walaumu mabadiliko ya Olimpiki ya Tokyo

  (GMT+08:00) 2019-11-06 09:05:41

  Maofisa wa riadha nchini Japan jana walilaumu uamuzi wa kuhamisha mbio za marathon na kutembea kwa kasi katika Olimpiki ya 2020 kutoka Tokyo hadi Sapporo, wakisema hatua hiyo haikuweka maslahi ya washindani mbele. Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa IOC mwezi uliopita iliamuru kuchukuliwa hatua hiyo baada ya kuona wanariadha wakitaabika na joto kali na hali ya unyevu katika mashindano ya mabingwa wa dunia yaliyofanyika Septemba huko Doha Qatar. John Coates, mkuu wa kamati ya uratibu ya IOC amesema wana wajibu wa kuweka mbele afya ya wanariadha. Uamuzi huo umekuwa wa kushtukiza kwa waandaaji wa Olimpiki ya Tokyo mwakani na jana Kazunori Asaba, mkuu wa mazoezi wa Shirikisho la vyama vya Riadha vya Japan (JAAF) amewaambia wanahabari kuwa hawakustahili kutoa uamuzi kama huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako