• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yatangaza hatua ya nne ya kupunguza utekelezaji wa makubaliano ya nyuklia

    (GMT+08:00) 2019-11-06 09:11:31

    Rais Hassan Rouhan wa Iran ametangaza kuwa kuanzia kesho Iran itaanza kutekeleza hatua ya nne ya kupunguza utekelezaji wake wa makubaliano ya nyuklia, kwa kuanza kuweka gesi kwenye mashinepewa zilizowekwa kwenye kinu cha Fordow.

    Rais Rouhani ameongeza kuwa Shirika la kimataifa la nishati ya Atomiki IAEA linafahamu uamuzi wa Iran, na litaendelea kuangalia shughuli za nyuklia za Iran. Hata hivyo amesema Iran itaheshimu tena makubaliano ya nyuklia, kama pande nyingine zilizosaini makubaliano hayo zitafanya hivyo.

    Tangu mwezi Mei Iran imechukua hatua tatu za kuongeza akiba ya nishati ya nyuklia na kurutubisha uranium kwa kiwango cha chini kuwa ya kiwango cha juu, na baadaye kuimarisha mashinepewa zake ili kuongeza akiba ya uranium iliyorutubishwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako