• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakurugenzi wa makampuni na wasomi kutoka nchi mbalimbali wapongeza mazingira ya kibiashara ya China

    (GMT+08:00) 2019-11-06 17:44:28

    Kongamano la pili la uchumi la kimataifa la Hongqiao limefanyika jana katika Kituo cha Maonyesho ya Shanghai. Kongamano hilo lenye kauli mbiu "Kufungua mlango, kufanya uvumbuzi na kunufaishana" ni sehemu muhimu inayounda Maonyesho ya pili ya Uingizaji Bidhaa kutoka Nje ya China (CIIE), na limeshirikisha wakurugenzi wa makampuni na wasomi kutoka nchi mbalimbali. Washiriki hao wamepongeza juhudi za China katika kuweka mazingira ya kibiashara yenye utulivu, usawa, uwazi na ufuanguji mlango pamoja na kuhimiza mageuzi ya kiuchumi.

    Mtaalamu wa Taasisi ya uchunguzi wa mambo ya uchumi wa dunia ya Peterson Bw. Gary Clyde Hufbauer amesema, China inashikilia kufanya uvumbuzi na mageuzi, huku ikitilia maanani ufunguaji mlango kwa pande zote, na kuweka mazingira ya kibiashara yenye usawa. Amesema,

    "Makampuni yote, bila kujali ni ya ndani au ya nje, au yanayomilikiwa na serikali ama binafsi, yote yanaweza kufanya ushirikiano wenye usawa. Kwa upande wa usimamizi, kuna mazingira ya kibiashara yenye usawa, kitu ambacho ni muhimu sana. 'Sheria ya uwekezaji kutoka nje' itakayotekelezwa mwakani inaonyesha juhudi za China kwenye sekta hiyo."

    Kampuni ya 3M ya Marekani imeleta bidhaa za aina mbalimbali za uvumbuzi na teknolojia ya kisasa kwenye maonyesho hayo. Ofisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Bw. Mike Roman ameona kuwa, rasilimali watu ya China ni sababu nyingine kuu ya kuvutia na kutuliza mitaji kutoka nje. Amesema,

    "China ina rasilimali kubwa ya watu, ambao wote wao ni hodari na wachapa kazi. Kampuni yetu imeanzisha vituo vya utafiti na maendeleo kwenye sehemu nne nchini China, ambako tutakuwa na fursa ya kupata wataalamu wa China. Aidha, kiwango cha elimu cha China kiko juu, hivyo China inatuvutia sana."

    Kampuni ya General Electric itaonyesha bidhaa za aina nyingi zenye uvumbuzi wa kisasa kwenye maonyesho hayo, pia itaonyesha ufumbuzi wao wa kutatua masuala ya nishati, na utengenezaji wa kisasa. Ofisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo anayeshughulikia mambo ya kimataifa Bibi Rachel Duan amesema,

    "Utandawazi ni wa kati ya pande mbili. Hivi karibuni kampuni yetu imemaliza mradi nchini Saudi Arabia, ambao ulijengwa na kampuni ya China, na vifaa vyao vya asili vinatoka Marekani, hivyo tunatakiwa kushirikiana kwa kutumia uwezo na mitaji ya dunia nzima badala ya nchi moja peke yake tu. Makampuni ya China na ya nchi nyingine yanaweza kufanya kazi zao kwenye sekta ya uvumbuzi wa awamu ijayo, kitendo ambacho ni ushirikiano halisi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako