• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Harambee Starlets kujitupa ugani Ijumaa itakapovaana na Zambia mechi ya kufuzu Olimpiki

    (GMT+08:00) 2019-11-07 09:11:40

    Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) limeamua kuwaondolea kiingilio mashabiki watakaofika uwanjani Kasarani kushabikia vidosho wa Harambee Starlets, katika mchuano wa kufuzu Michezo ya Olimpiki Tokyo. Starlets watamenyana na vipusa wenzao kutoka Zambia kesho Ijumaa, katika juhudi za kujikatia tiketi ya kushiriki michezo hiyo ya Olimpiki itakayofanyika nchini Japan mwaka ujao. Mchuano huo utakaosimamiwa na refa Shamirah Nabaddah akisaidiwa na waamuzi wenzake wazawa wa Uganda Jane Mutonyi, Nakitto Nkumbi na Florence Ayaro, hadi kufikia mwishoni mwa wiki iliyopita, ulikuwa ukikabiliwa na ukata wa fedha uliotishia kusambaratisha maandalizi ya Starlets baada ya FKF kuvunja kambi ya mazoezi ya vipusa hao, wanaonolewa na kocha David Ouma. Starlets watajibwaga ugani siku tatu tu baada ya kupepetwa 3-1 na chipukizi wa Kenya wasiozidi umri wa miaka 15, katika mechi ya kirafiki iliyofanyika uwanjani Nyayo, Nairobi, juzi Jumanne. Chini ya mkufunzi Ouma, Starlets wako pua na mdomo kuweka historia ya kufuzu Michezo ya Olimpiki kwa mara ya kwanza, iwapo watazamisha chombo cha Zambia baada ya michuano ya mikondo miwili. Mchuano wa marudiano kati ya Kenya na Zambia utachezwa jijini Lusaka Jumatatu ijayo, Novemba 11.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako