• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu sita wafariki baada ya kupigwa na radi nchini Uganda

  (GMT+08:00) 2019-11-08 18:41:11

  Watu sita wamefariki na wengine 11 kujeruhiwa vibaya baada ya kupigwa na radi katika wilaya ya Pader, kaskazini mwa Uganda hapo jana.

  Kamanda wa Polisi Tom Bainomugisha ameliambia Shirika la Habari la China Xinhua kuwa, watu hao walikuwa wamekusanyika chini ya mti mkubwa wakijikinga na mvua ya asubuhi wakati radi ilipopiga.

  Amesema radi ni kitu cha kawaida katika eneo hilo, na mwezi Septemba, wakulima wanne walifariki baada ya kupigwa na radi katika wilaya ya Kanungu iliyoko kusini magharibi mwa Uganda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako