• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM yaonya dharura zinazoweza kutokea baada ya mafuriko nchini Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2019-11-09 17:05:41

    Umoja wa Mataifa umeonya juu ya dharura zinazoweza kutokea baada ya mafuriko nchini Sudan Kusini.

    Mratibu wa Mambo ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, Alain Noudehou, jana alitaka kutolewa kwa dola za Kimarekani milioni 61.5 kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu na kusaidia watu waliopo kwenye mafuriko makubwa ambayo yameathiri theluthi moja ya kaunti zote nchini.

    Naye msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, amesema Mratibu wa Misaada ya Dharura wa Umoja wa Mataifa Mark Lowcock atatenga kiasi cha dola milioni 15 kutoka kwenye Mfuko wa Mwitikio wa Dharura wa Umoja wa Mataifa ili kuitikia haraka mafuriko hayo. Fedha hizo zitatumika kuwasaidia watu laki 6.2 waliopo maeneo yaliyoathrika zaidi kwa kuwapatia makazi, huduma za afya, chakula, maji, vifaa safi na salama pamoja na misaada mingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako