• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kimbelembele cha kung'ang'ania penalti chamuingiza kwenye adhabu kali mchezaji wa Club Brugge

    (GMT+08:00) 2019-11-11 08:55:31

    Klabu bingwa Ubelgiji, Club Brugge, imemuadhibu vikali mchezaji wake Mbaye Diagne kwa kupoteza penalti wakati wa mechi dhidi ya Paris Saint-Germain katika pambano la Ligi ya Mabingwa mnamo Jumatano, Novemba 6 usiku. Brugge walikuwa na nafasi nzuri ya kusawazisha kombora la Mauro Icardi katika dakika ya 76, baada ya kutunikiwa penalti huku Diagne, katika hali ya utata akisisitiza kupiga mkwaju huo lakini akapoteza. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, alimzuia kiranja wa Brugge, Hans Vanaken kuchukua jukumu hilo, kabla ya kombora lake kupanguliwa na Keylor Navas. Tukio hilo lilimfanya meneja wa klabu hiyo Philippe Clement, kupandwa na mori na kuthibitisha kuwa fowadi huyo wa Senegal ataadhibiwa kwa kutoshirikishwa katika kikosi cha Club Brugge kitakachovaana na Royal Antwerp katika mechi ya ligi. Pia alisema kutakuwa na faini kubwa ya fedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako