• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • MASUMBWI: Bondia afariki dunia muda mfupi tu baada ya kumaliza mazoezi

    (GMT+08:00) 2019-11-11 08:56:18

    Bondia Dwight Ritchie raia wa Australia amefariki, huko jijini Melbourne, muda mfupi baada ya kumaliza mazoezi yake ya kawaida. Promota aliyekuwa akisimamia mapambano ya Ritchie, Jake Ellis, amethibitisha kifo cha bondia huyo ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 27. Ritchie alikuwa ameshacheza mapambano 21, ambapo kati ya hayo alipoteza mawili tu, moja likiwa ni lile la hivi karibuni dhidi ya Tim Tszyu kuwania taji la IBF Australia kwenye uzito wa 'Super-welterweight' mapema mwezi Agosti. Katika mazoezi hayo Ritchie alikuwa anafanya na bondia Michael Zerafa, ambaye anajiandaa kwa pambano la marudiano na Jeff Horn, ambaye ni bingwa wa zamani wa WBO Welterweight.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako