• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NETIBOLI: Ligi ya Muungano ya Netiboli imezinduliwa

    (GMT+08:00) 2019-11-11 17:53:29
    Mashindano ya ligi ya Muungano ya mpira wa Netiboli yamefunguliwa jana na mkuu wa wilaya ya Kaskazini B Rajab Ali Rajab, kwenye kiwanja cha Gymkhana. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa ligi hiyo, mkuu huyo wa wilaya alizitaka timu shiriki kucheza kwa nidhamu ili kuendelea kudumisha Muungano. Alisema kucheza kwa nidhamu na heshima ndio msingi wa kupata maendeleo kupitia mchezo huo ili kuwasaidia kufikia malengo yao. Aidha alisema yupo tayari kushirikiana na uongozi wa chama cha mchezo huo katika kupambana na changomoto walizonazo ili kuhakikisha wanamaliza salama mashindano hayo. Mashindano hayo yanashirikisha timu 15 kutoka Tanzania bara na Zanzibar, wanaume timu nne na wanawake timu 11.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako