• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kitendo cha ofisa wa Marekani kina hila ya kisiasa

    (GMT+08:00) 2019-11-11 20:16:12

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, habari zinazosema China imeweka vifaa vya kusikiliza mambo yanayozungumzwa katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika si za kweli.

    Hivi karibuni, Marekani ilidai kuwa, serikali ya China imeiba takwimu za Umoja wa Afrika kwa miaka mitano kwa kutumia vifaa vya Huawei. Bw. Geng amesema, taarifa hizo zimepingwa na viongozi wengi wa nchi za Afrika na mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika na kuongeza kuwa, China na Afrika ni marafiki na ndugu, na ushirikiano kati yao ni wazi na bila ya nia binafsi.

    Wakati huohuo, Bw. Geng amemkosoa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo kwa kuwa na fikra ya vita baridi, akikataa mfumo wa ujamaa wenye umaalum wa kichina na kutenganisha uhusiano kati ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC na Wachina ili kutimiza malengo yake binafsi ya kisiasa, jambo ambalo hakika litashindikana.

    Bw. Geng amesema katika miongo saba iliyopita, CPC imewaongoza Wachina kupata maendeleo makubwa ya kihistoria, na uongozi wa CPC ni chaguo la wananchi. Ameongeza kuwa China ina imani, njia, nadharia, mfumo na utamaduni wake, na itaendelea kufuata mfumo wa ujamaa wenye umaaluma wa kichina na kupata mafanikio mengine mapya

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako