• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yataja Marekani ni chanzo cha mgogoro wa nyuklia ya Iran

  (GMT+08:00) 2019-11-12 18:42:41

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo amesema, Marekani kujitoa kwenye makubaliano ya pande zote ya mpango wa nyuklia wa Iran na kuiwekea Iran vikwazo ni chanzo cha mgogoro wa nyuklia ya Iran.

  Amesema Marekani inapaswa kuacha vitendo vya makosa na kuweka mazingira ya kutuliza mgogoro katika eneo hilo.

  Habari zinasema, Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) jana lilitangaza ripoti mpya kuhusu usimamizi na ukaguzi kwa Iran. Mawaziri wa Uingereza, Ufaransa na Ujerumani na mjumbe wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia sera ya diplomasia na usalama walitoa taarifa ya pamoja na kusema wanafuatilia kwa karibu uamuzi wa Iran wa kuanzisha tena usafishaji wa uranium huko Fordo, wakizingatia mifumo yote ya makubaliano ya pande zote na kutatua suala la kutekeleza makubaliano hayo kwa Iran.

  Bw. Geng Shuang amesema, China inaiunga mkono IAEA kutekeleza majukumu yake kwa haki na kuendelea kushirikiana na pande mbalimbali kuhimiza suala la nyuklia la Iran kutatuliwa kwa njia ya kidiplomasia na ya kisiasa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako