• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sarafu ya Kenya yaimarika

    (GMT+08:00) 2019-11-12 19:09:55

    Sarafu ya Kenya inaendelea kunufaika kutokana na kuongezeka kwa mapato ya sarafu ya dola katika soko la hisa na mapato kutoka kwa waagizaji.

    Kulingana na Benki Kuu ya Kenya ,benki za kibiashara zilibadilisha sarafu ya Kenya kwa wastani wa Sh102.50 dhidi ya dola ya Marekani jana,ikilinganishwa na wastani wa Sh102.81 tarehe 8,ijumaa iliyopita,baada ya kufika ubadilishanaji wa Sh102 tarehe 7 Novemba ilipobadilishwa kwa Sh102.95.

    Katika taarifa ya kila wiki,Benki Kuu ya Kenya ilisema shilingi ya Kenya ilikuwa imara dhidi ya sarafu kuu za kimataifa na kikanda katika wiki iliyoisha tarehe 7 novemba.Ilibadilishwa kwa Sh102.95 kwa kila dola moja,ikilinganishwa na Sh103.21 tarehe 31 Oktoba.

    Aidha benki Kuu ilisema,akiba ya fedha za kigeni ilisalia kuwa imara ikiwa na Sh914.53 bilioni ($8931 milioni), kufikia mwisho wa wiki jana,kutoka Sh917.61 bilioni ($8961 milioni) wiki kabla ya hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako