• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Magufuli kuhimiza watanzania kuondokana na utegemezi kwa wahisani

  (GMT+08:00) 2019-11-13 08:33:54

  Rais John Magufuli wa Tanzania amesema serikali yake itachukua hatua zote zinazohitajika ili kuhakikisha Tanzania inaondokana na kasumba ya kutegemea wahisani.

  Akiongea kwenye uzinduzi wa kitabu cha wasifu wa aliyekuwa Rais wa Tanzania Bw. Benjamin Mkapa, Rais Magufuli amesema kama Tanzania ikitaka kusimamia vizuri raslimali zake, inatakiwa kuondokana na utegemezi kwa wahisani. Amesema Tanzania ina nafasi ya kupunguza utegemezi huo, kama itaongeza usimamizi kwenye ukusanyaji wa kodi, kusimamia vizuri maliasili zake na kutekeleza miradi ya ujenzi.

  Wiki iliyopita kwenye mkutano wa 18 kati ya nchi za Afrika na mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa nchi za Ulaya Kaskazini, Rais Magufuli alizitaka nchi za Afrika kujiangalia upya na kuangalia nafasi yake kwa kurekebisha zilipokosea.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako