• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda tayari kushindana na mashirika mengi ya ndege Afrika

    (GMT+08:00) 2019-11-13 19:43:49

    Serikali ya Uganda imeagiza ndege mbili aina ya Airbus ili kuboresha biashara ya usafiri wa anga nchini humo.

    Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Uganda (UCAA) Bw David Kakuba amesema, Uganda inatarajiwa kupata Airbus mbili aina ya A 330 ifikapo mwaka ujao.

    Aidha Bw Kakuba ameongeza kuwa ndege hizo zinatarajia kufanya safari zake katika nchi za Uingereza, India na China.

    Amewataka raia wa Uganda kuunga mkono shirika hilo la ndege badala ya kulizungumzia vibaya. Amesema kila Mganda anapaswa kujivunia vya Uganda kwasababu zitaongeza utalii na hatimaye nchi kufanikiwa kuongeza pato la Taifa."

    Awali waziri wa Kazi na uchukuzi wa Uganda Bi Monica Azuba alisema ndege hizo zinatarajiwa kuwasili mwaka 2020 na kuongeza kuwa kwa sasa shirika hilo lina ndege zaidi ya 10.

    Alisema ndege hizo zitaleta ushindani mkubwa kwa safari za kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako