• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Uingereza kuchunguza shambulizi dhidi ya ofisa wa serikali ya utawala maalum wa Hong Kong

    (GMT+08:00) 2019-11-15 18:53:28
    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China inalaani vikali shambulizi dhidi ya mkurugenzi wa idara ya sheria ya Hong Kong lililotokea nchini Uingereza, na kuitaka nchi hiyo kufanya uchunguzi dhidi ya shambulizi hilo mara moja na kuwakamata wahusika na kuwafikisha mahakamani.

    "Hali iliyopo imeonesha kuwa, watu wanaopinga serikali kuu ya China na kufanya vurugu mkoani Hong Kong ni wahalifu. Vitendo vyao vimevuka mpaka wa sheria na utamaduni. Kitendo cha kushambulia maofisa wa serikali kinapaswa kuzuiliwa na kuadhibiwa. Wahalifu hao wataharibu ustawi na usalama wa Hong Kong na pia kuiletea jumuiya ya kimataifa ikiwemo Uingereza usumbufu na uharibifu mkubwa."

    Bw. Geng pia amesema, China inaitaka Uingereza kulinda usalama na heshima ya wachina wote nchini humo. Pia inaihimiza Uingereza iwe makini na masuala yanayohusiana na Hong Kong, kuacha kutoa habari isiyo sahihi, kuacha uchochezi na kuacha kuingilia mambo ya ndani ya Hong Kong.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako