• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Biashara katika mfumo wa malipo ya kodi kuongezeka

    (GMT+08:00) 2019-11-15 19:21:54

    Kenya imepanua wigo wa mradi wa nembo za ushuru za kielektroniki kuyafikia maeneo mengine mapya ya uzalishaji ili kuiwezesha mamlaka kuziingiza biashara nyingi zaidi katika mfumo wa malipo ya kodi.

    Hivi sasa , juisi, vinywaji vya kuongeza nguvu, soda na vinywaji vingine visivyo na vilevi vinavyozalishwa au kuingizwa nchini humo vitakuwa na nembo maalumu ambayo inatolewa na Mamlaka ya Mapato ya Kenya (KRA) pekee kwa wazalishaji walioidhinishwa.

    Kamishna wa Mkuu wa KRA, James Mburu aliandika kupitia ukurasa wake wa Twitter juzi kwamba kuanzia leo Jumatano itakuwa mwisho wa uwekaji wa nembo hizo kwenye bidhaa.

    Kamishna wa Kodi za Ndani KAR, Elizabeth Meyo alisema hivi sasa Kenya ina wazalishaji zaidi ya 130 na waingizaji wa maji ya chupa, juisi, soda, vinywaji vya kuongeza nguvu (Energy drinks) na vinywaji vingine visivyo na vilevi ambao wameshasajiliwa katika mfumo wa kielektroniki wa Utambuzi wa Bidhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako