• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapanga kukamilisha ujenzi wa kituo cha anga za juu mwaka 2022

    (GMT+08:00) 2019-11-18 08:24:03

    Msanifu mkuu wa programu ya kutuma wanaanga kwenye anga za juu ya China Bw. Zhou Jianping, amesema China inapanga kukamilisha ujenzi wa kituo cha anga za juu na kuanza kukitumia mwaka 2022.

    Akizungumuza kwenye Jukwaa la nne la Uhandisi wa Kuzingatia Mahitaji ya Binadamu (HFE) lililofanyika wikiendi katika chuo kikuu cha Sun Yat-sen mjini Guangzhou, Bw. Zhou amesema kituo hicho cha anga za juu kinatarajiwa kuwa na uzito wa tani 100 na kuweza kuchukua wanaanga watatu. Lengo kuu la ujenzi wa kituo hicho ni kuiwezesha China kuendeleza kwa kujitegemea teknolojia ya safari za muda mrefu za kutuma wanaanga kwenye anga za juu karibu na Dunia, na kuwa na uwezo wa kufanya majaribio ya kisayansi ya muda mrefu kwenye anga za juu, na kutumia raslimali za anga za juu.

    Kituo hicho kitajengwa kuwa jukwaa kuu la China kwa ajili ya utafiti wa sayansi ya anga za juu, kwa lengo la kuendeleza teknolojia za kujenga na kuendesha vyombo vikubwa vya anga za juu na teknolojia zinazohakikisha maisha na afya ya wanaanga wanaokaa muda mrefu kwenye obiti, na ujenzi wa maabara ya anga za juu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako