• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashindano ya ujasiriamali barani Afrika yamalizika

    (GMT+08:00) 2019-11-18 16:16:33

    Fainali za mashindano ya ujasirimali barani Afrika na mkutano wa wajasiriamali barani humo zilizofadhiliwa Mfuko wa Jack Ma na Mfuko wa Alibaba wa China zimemalizika hivi karibuni katika mji mkuu wa Ghana, Accra. Washindi 10 wa mashindano hayo yaliyowashirikisha zaidi ya vijana elfu 10 kutoka nchi zaidi ya 50 za Afrika walipewa tuzo ya dola milioni moja za kimarekani ambazo zilitolewa na Mfuko wa Jack Ma wa Ujasiriamali Barani Afrika.

    Jack Ma ambaye ni mwanzilishi wa Kampuni ya Alibaba la China ni tajiri mkubwa zaidi nchini China kwa kumiliki mali zenye thamani ya dola bilioni 38.58 za kimarekani. Sasa amestaafu kazi nyingine na kujishughulisha tu na hisani. Mwezi Agosti mwaka jana, Bw. Ma alianzisha Mfuko wa Ujasiriamali Barani Afrika, na kila mwaka anatoa dola milioni moja za Kimarekani kwa washindi wa Mashindano ya Ujasiriamali barani humo, ili kuwahamasisha vijana kufanya ujasiriamali na kujiendeleza. Licha ya kutoa fedha, mfuko huo pia unatoa mafunzo, ushirikiano wa kibiashara na kuunga mkono shughuli nyingine za wajasiriamali wa Afrika.

    Washindi wa mashindano ya mwaka huu wanatoka Misri, Nigeria, Liberia, Rwanda na Cote d'Ivoire, na wanafanya kazi za mauzo, kilimo, matibabu, mapambo, viatu na vifaa ya utafiti wa sayansi. Bw. Ma amesema, Afrika ina rasilimali na fursa nyingi za kufanya ujasiriamali, vijana wanapaswa kujitokeza kufanya majaribio na uvumbuzi, ili kubadilisha bara hilo. Anasema, "Watu walioshiriki kwenye mashindano hayo ni mbegu za ujasiriamali za Afrika, na wataamsha wengine kubadilisha maisha na kutimiza ndoto zao. Kama majasiri hao wa kibiashara wakipata mafanikio, majasiri wengine wengi wa kibiashara wataibuka. Hivyo tunatarajia kuwa mafanikio yao yataleta matumaini mapya kwa Afrika.

    Hafla ya kumalizika kwa mashindano hayo ilihudhuriwa na rais Nana Addo Dankwa Akufo-Addo wa Ghana, katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon, na balozi wa China nchini Ghana Bw. Wang Shiyan. Rais Akufo-Addo amemshukuru Bw. Ma kwa kuanzisha Mfuko wa Ujasiriamali Barani Afrika, akisema, "Tunapaswa kujitahidi kujenga Afrika kwa pamoja, ili kurithisha mali kwa vizazi vya baadaye. Hatuwezi kukosa fursa hii, na tunatakiwa kuendeleza nia ya wanaviwanda wa Afrika, kuwasaidia kujiongezea uwezo, na kuwaanzishia mazingira mazuri ya kibiashara, ili kuhimiza maendeleo ya uchumi. Naamini kuwa tunaweza kujenga Ghana na Afrika yenye ustawi na imani zaidi, na kubadilisha Afrika kwa kuvutia uwekezaji wa nje na kufanya biashara na nchi za mabara mengine duniani."

    Mjasiriamali kutoka Nigeria bibi Temie Giwa Tubosun ni mshindi wa mashindano hayo. Kampuni yake ya Benki ya Maisha inasaidia hospitali kutafuta vifaa muhimu kupitia data kubwa na teknolojia nyingine za kisasa. Hadi sasa kampuni yake imeokoa maisha ya watu zaidi ya 5,300. Bibi Giwa anasema, "Nafurahi sana, kwani siku zote naamini kuwa tunapaswa kuwahamasisha wanawake wa Afrika waendelee kuwa na ndoto kubwa ya kutatua masuala ya kijamii. Sasa wamefanya hivyo. Jambo linalonifurahisha zaidi ni kwamba, mshindi wa "jasiri wa kibiashara" wa mwaka huu ni mwanamke, ni mwanamke kutoka Afrika. Hadithi yangu itawahamasisha wanawake wengine, na wataongoza kutatua masuala na kuwa mifano mipya."

    Habari zinasema Mashindano ya Ujasiramali Barani Afrika ya mwaka ujao yanatarajiwa kuoneshwa katika televisheni, ili kuwahamasisha vijana wengi zaidi kufanya ujasiriamali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako