China imeitaka Marekani ishughulikie suala la Taiwan kwa uangalifu na mwafaka na isiongeze mvutano mpya kwenye Mlango Bahari wa Taiwan.
Hayo yamesemwa na waziri wa ulinzi wa China Wei Fenghe alipokutana na mwenzake wa Marekani Mark Esper leo mjini Bangkok. Wei pia amesema China siku zote inapenda kutatua kwa amani suala la Taiwan, lakini kamwe haitavumilia tukio baya la Taiwan kujitenga na China. Kuhusu Bahari ya Kusini ya China, Wei amesema China ina nia thabiti ya kulinda mamlaka ya ardhi na maslahi yake katika eneo hilo la bahari, na inaitaka Marekani iache kuonyesha nguvu yake na kuchochea mvutano kwenye Bahari ya Kusini.
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya China Wu Qian amesema mkutano kati ya mawaziri hao ulikuwa mzuri na wa kiujenzi, na pande hizo mbili zimekubaliana kuwa uhusiano mzuri kati ya majeshi yao si tu utanufaisha nchi hizo na majeshi, bali pia utachangia amani na utulivu wa kikanda na wa dunia. Ameongeza kuwa mawaziri hao wameahidi kufanya mipango kuhusu mawasiliano makubwa kati ya majeshi ya nchi hizo mwakani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |