• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya mitaji kutoka nje nchini China yaongezeka kwa asilimia 6.6 katika miezi kumi ya mwanzo ya mwaka huu

    (GMT+08:00) 2019-11-18 19:14:05

    Takwimu zilizotolewa jana na wizara ya biashara ya China zimeonyesha kuwa, kuanzia mwezi Januari hadi Oktoba mwaka huu, idadi ya matumizi ya mitaji kutoka nje nchini China imefikia dola bilioni 107.3 za kimarekani, na kuongezeka kwa asilimia 6.6.

    Mkuu wa idara ya mitaji ya nje katika wizara ya biashara ya China Bw. Zong Changqing amesema, uwekezaji kutoka maeneo ya Hong Kong, Macao, na nchi za Singapore na Korea Kusini umeongezeka, huku uwekezaji kutoka nchi zilizoko kwenye "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na Umoja wa nchi za Asia Kusini Mashariki nayo pia ukiongezeka.

    Amesema China ina uwezo wa kuvutia uwekezaji kutoka nje, na wawekezaji kutoka nchi mbalimbali wana imani kubwa ya kuwekeza nchini China, na malengo ya China ya mwaka huu katika kutuliza mitaji ya nje yanatarajiwa kutimia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako